Watumishi wa Ataba mbili tukufu wanaomboleza kifo cha Zaharaa (a.s)

Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wameomboleza kifo cha bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu.

Matembezi ya kuomboleza yameanzia ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakapitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili, huku wanaimba kaswida za kuomboleza zinazo amsha hisia za huzuni na majonzi katika nafsi za waumini.

Baada ya kuwasili katika haram ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s) wakafanya majlisi iliyopambwa na kaswida mbalimbali zilizokua na tenzi zinazo eleza dhulma aliyofanyiwa bibi Zaharaa (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: