Kitengo cha maarifa kinafanya semina kuhusu uhakiki wa nakala-kale na faharasi

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya semina kuhusu uhakiki wa nakala-kale na faharasi.

Mkufunzi wa semina Shekhe Saaduni Saray amesema “Semina imeandaliwa na kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa, wamefundishwa masomo ya msingi katika elimu ya uhakiki nakala-kale, wanafunzi wa hauza za Karbala na Najafu wameshiriki kwenye semina hiyo”.

Akaongeza kuwa “Semina inalenga kupata wahitimu wenye uwezo wa kufanya uhakiki wa nakala-kale na uwezo wa kuzisoma na kuzikarabati kwa kuandika upya sehemu zilizofutika, na kuwaandaa kufanya kazi za turathi kwenye taasisi za uhakiki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: