Katika kumbukumbu ya kifo cha Zaharaa.. chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya majlisi ya kuomboleza

Chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Mahadi Bayati, baada yake Shekhe Jafari Waailiy akapanda kwenye mimbari.

Shekhe ameongea kuhusu dhulma aliyofanyiwa bibi Zaharaa (a.s) baada ya kifo cha baba yake, na jinsi alivyo pambana kulinda bendera ya utume na uimamu, jambo ambalo lilisababisha kuongeza kudhulumiwa kwake.

Majlisi ikahitimishwa kwa kaswida na tenzi za kuomboleza zilizo amsha hisia za majonzi na huzuni kwa waumini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: