Kitengo cha Dini kinafanya matembezi ya kuomboleza kifo cha Fatuma (a.s)

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimefanya matembezi ya kuomboleza kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu.

Msimamizi wa matembezi hayo Shekhe Haidari Aaridhwi amesema “Matembezi haya ni sehemu ya harakati za kitengo” akabainisha kuwa “Watu kutoka wilaya tofauti wameshiriki kwenye matembezi haya”.

Akaongeza kuwa “Waombolezaji wamebeba bendera na vitambaa vilivyo andikwa jumbe mbalimbali kuhusu tukio hilo, huku wakiimba kaswida za kuomboleza kifo cha mtoto wa Mtume (a.s) na namna alivyo jitolea kusimamisha Dini na kupambana na batili”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: