Ugeni kutoka chuo cha Imamu Swadiq (a.s) umetembelea vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu

Ugeni kutoka chuo cha Imamu Swadiq (a.s) katika mji wa Najafu, umetembelea Atabatu Abbasiyya na kuangalia sehemu mbalimbali za Ataba.

Kitengo cha uhusiano kimeandaa ratiba kamili ya wageni hao, imehusisha kutembelea Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na kutembelea vitengo tofauti vya Ataba hizo.

Ziara hii ni sehemu ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, aidha wametembelea pia makumbusho ya Alkafeel na baadhi ya maeneo muhimu.

Mkufunzi wa chuo hicho Dokta Sajaad Kindi amesisitiza umuhimu wa kutembelea malalo za Ahlulbait (a.s) na kufungamana nazo, kwa sababu ziara hizi humjenga mtu kiroho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: