Atabatu Abbasiyya imefanya kikao cha kujadili amani ya Ataba tukufu

Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kikao cha kujadili amazi ya Ataba na mazuwaru wake.

Kikao hicho kimeongozwa na mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Afdhalu Shami na kuhudhuriwa na viongozi wa kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, idara ya ulinzi na taarifa, idara ya sheria na idara ya ufuatiliaji.

Katika kikao hicho wamejadili usalama wa mji mkongwe wa Karbala na maeneo yanayozunguka Atabatu Abbasiyya tukufu.

Sayyid Shami amesifu utendaji wa watumishi wa Ataba kitengo cha usalama kwa namna walivyo walinda mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na akawataka waendelee kufanya hivyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: