Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya warsha ya viongozi wa idara na vitengo katika Atabatu Abbasiyya iliyopewa jina la (Kutambua changamoto na utatuzi wake).
Mkufunzi wa warsha hiyo Sayyid Ridhwa Al-Abuudi amesema “Warsha hii inalenga kuwajengea uwezo wa kubaini changamoto na kuzitatua kwa njia za kielimu, viongozi wa idara. Sambamba na kuwafundisha ubunifu kwenye utendaji wao na utatuzi wa changamoto”.
Warsha ilikua na mada nyingi, miongoni mwa mada zake ni “Utambuzi wa changamoto, hatua za kutatua changamoto, mfano wa changamoto, mti wa mifano ya kubaini changamoto, pamoja na kuwapa muongozo wa utendaji bora na utekelezaji wa majukumu”.
Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu hufanya warsha na semina za kuwajengea uwezo watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.