Kitengo cha habari: Tunategemea mradi unaolenga kukusanya vielelezo muhimu vya kihistoria

Kitengo cha habari na utamaduni kupitia kituo cha upigaji wa picha nakala-kale na faharasi kimetangaza kuwa kinategemea miradi ya kukusanya vielelezo muhimu.

Kiongozi wa kitengo cha vielelezo katika kituo Sayyid Muhammad Baaqir Zubaidi amesema kuwa “Mradi wa (Turathi zako ni amana) unalenga kuhamasisha familia za wairaq kutoa vielelezo vya kihistoria walivyo navyo kutoka kwa mababu zao, vinavyo elezea historia ya Iraq na mambo yaliyotokea kwa lengo la kulinda historia ya taifa hili isipotee”.

Akabainisha kuwa “Mradi huu umepata muitikio mkubwa sana baada ya miaka miwili ya kuanzishwa kwake kutoka kwenye mikoa tofauti ya Iraq, tumefanikiwa kukusanya karibu vielelezo (3500) na bado unaendelea kuwa na mwitikio mzuri”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Zubaidi “Vielelezo muhimu vitakabidhiwa kwa Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kutunzwa” akafafanua kuwa “Vielelezo vingi ni vya zama za utawala wa Othumaniyya na vinavyo husu historia ya mji wa Karbala na ujenzi wa Ataba tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: