Kuhitimisha kongamano la Shahada awamu ya kumi na mbili

Kongamano la Shahada awamu ya kumi na mbili limehitimishwa katika chuo kikuu cha Waasit, kongamano hilo limeandaliwa na taasisi tofauti kwa kushirikiana na Ataba mbalimbali, ikiwemo Atabatu Abbasiyya tukufu.

Katika kongomano hilo kulikua na vikao-darasa (nadwa) asubuhi na jioni, maenyesho ya vitabu, mauwa na vikao vya usomaji wa Qur’ani, zaidi ya watafiti 60 kutoka vyuo vikuu tofauti vya Iraq wameshiriki.

Watumishi wa Atabatu Abbasiyya kutoka kitengo cha Habari na utumishi wameshiriki kutoa mihadhara kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wamejitokeza kwa wingi kwenye kongamano hilo.

Kongamano limedumu kwa muda wa siku kumi na mbili, limepambwa pia na igizo la bibi Fatuma Zaharaa (a.s) lililo onyesha historia yake takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: