Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imewapa mtihani wa kusoma Qur’ani na kuhifadhi wanafunzi 170 kutoka Kijiji cha Ghadiir.
Kiongozi wa Maahadi Ustadhat Mannaar Aljaburi amesema “Kutokana na kufika mwisho wa mwaka, tumeona tuwape mtihani wanafuni kutoka Kijiji cha Alghadiir wa kusoma Qur’ani tukufu na kuhifadhi kulingana na kiwango cha kila mshiriki”.
Mtihani huo umesimamiwa na walimu watatu kutoka Maahadi, akasisitiza kuwa “Umuhimu wa mitihani hii, inasaidia kujenga uwezo wa wanafunzi na kusahihisha makosa yao sambamba na kushajihisha kuendeleza vipaji vya usomaji wa Qur’ani kwenye vituo tofauti hapa nchini”.