Kitengo cha maadhimisho kimemaliza shughuli za msimu wa huzuni za Fatwimiyya

Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kimemaliza msimu wa kuomboleza kifo cha Fatuma (a.s).

Rais wa kitengo Sayyid Aqiil Alyasiri amesema “Program zote zilizo andaliwa na kitengo katika kuomboleza kifo cha mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu, zimekamilika”.

Akaongeza kuwa “Program hizo zimedumu kwa zaidi ya siku 20, zilikua na vipengele vingi, yakiwemo maigizo na ufanyaji wa majlisi za kuomboleza ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein na Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akabainisha kuwa “Wafuasi wote wa Ahlulbait (a.s) huomboleza msiba huu, baadhi ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya wamefanya majlisi za kuomboleza katika mji wa Mosul, Bagdad, Basra na miji mingine”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: