Kujenga uwezo wa watumishi wake.. Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya inafanya warsha ya kujenga uwezo

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya imefanya warsha ya kuwajengea uwezo watumishi wake na wahadhiri, yenye anuani isemayo (Njia za lazima kwa mkufunzi).

Mhadhiri wa warsha hiyo alikua ni Dokta Hassan Aljudhailiy, ameongea kuhusu mbinu muhimu za mkufunzi wwenye mafanikio, sambamba na kwenda pamoja na maendeleo ya kisasa kwa kujifunza kila jambo jipya.

Idara inaendelea kufanya warsha kwa ajili ya kufikia malengo yaliyowekwa katika mradi wa mbeba ujumbe wa Zainabiyya unaolenga kuwajengea uwezo wanafunzi wa shule zilizopo katika mkoa mtukufu wa Karbala.

Semina na warsha hufanywa kila siku ya Jumapili kwa muda wa saa tatu, na zitaendelea kwa miezi mitatu mfululizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: