Huu ni wakati wa ufunguzi wake.. mradi wa Sardabu ya Imamu Hussein (a.s) umekamilika kwa asilima kubwa

Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, kimesema kuwa mradi wa Sardabu ya Imamu Hussein (a.s) unaojengwa katikati ya haram ya Abbasi, umekamilika kwa asilimia kubwa.

Rais wa kitengo cha uhandisi Dhiyaau Swaaigh amesema “Mradi upo katika hatua za mwisho, umepita hatua mbalimbali za utekelezwaji ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nguzo 12 za zege chini ya ardhi”.

Akaongeza kuwa “Tumeanza hatua ya pili ya mradi ambayo inahusisha ufungaji wa mifumo tofauti ndani ya Sardabu, kama vile mfumo wa umeme, viyoyozi, zimamoto, hatua hiyo pia imeshakamilika, tupo katika matengenezo ya mwisho ya kuweka vioo, mapambo, kuandika aya za Qur’ani kwenye kuta, hadi sasa kazi imekamilika kwa asilimia 95”.

Siku zijazo litawekwa dirisha takatifu ndani ya Sardabu, kwa mujibu wa maelezo ya Swaaigh, akasisitiza kuwa mradi huu utakamilika na kufunguliwa kabla ya Ramadhani ijayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: