Miongoni mwa maandalizi ya kongamano la Ruhu-Nubuwwah.. kamati ya elimu imefanya kikao kujadili mada zitakazowasilishwa kwenye kongamano hilo awamu ya tano.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi Dokta Amaali Aali-Haidari amesema “Kamati ya maandalizi ya kongamano la Ruhu-Nubuwwah awamu ya tano imefanya kikao cha pili kujadili mada zitakazo wasilishwa, ili waweze kutangaza mada zilizo shinda katika mchujo huo”.

Akaongeza kuwa “Mada zilizo wasilishwa ziko (149) kutoka ndani na nje ya Iraq, zitachaguliwa mada (20) zitakazo wasilishwa kwenye kongamano, kisha zitachujwa hadi tupate mada zatu bora”, akabainisha kuwa “Kongamano litafanyika hivi karibuni na maandalizi yapo hatua za mwisho”.

Kamati ya majaji wanaochuja mada zitakazo shiriki kwenye kongamano inaundwa na wajumbe tisa kutoka Bagdad, Najafu na Basra kwa mujibu wa maelezo ya Aali-Haidari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: