Kituo cha utamaduni wa familia kinafanya program ya kusaidia mwanamke mtumishi

Kituo cha utamaduni wa mwanamke chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya program ya (kuwajengea uwezo wenye vipaji) kutoka shule ya sekondari (upili) ya Amuriyya na Shahidi Abi-Maaliy.

Program hiyo inafanywa ndani ya ukumbi wa Sidri ikiwa na anuani isemayo (Furaha yako hutengenezwa na fikra zako) chini ya uhadhiri wa Adhraa Ahmadi, amezungumza mada isemayo (utambuzi wa vitendo), washiriki wamepewa nafasi ya kuuliza maswali kisha zawadi zikatolewa kwa waliofaulu.

Kulikua na mada isemayo (unaona nini) iliyowasilishwa na Sundusi Muhammad huku ikipambwa na kuangalia baadhi ya picha zenye maana tofauti na kufafanuliwa.

Program ikahitimishwa na kipengele kisemacho (kutoka kwenu hadi kwenu) kilicho husisha maswali na majibu kutoka kwa washiriki.

Program hii inalenga watumishi kwa lengo la kujenga uwezo wao na kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: