Kitengo cha habari kinafanya semina ya kuhakiki nakala-kale

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimefanya semina ya kuhakiki nakala-kale.

Rais wa kitengo cha uhakiki katika kituo cha kuhuisha turathi Sayyid Dhiyaau Karbalai amesema “Semina imepambwa na masomo ya msingi katika elimu ya uhakiki wa nakala-kale, na namna ya kuzilinda na kunufaika nazo, washiriki walikua ni wanafunzi wa hauza katika mji wa Karbala”.

Akaongeza kuwa “Semina hii inalenga kueneza elimu ya uhakiki kwa ajili ya kuongeza juhudi ya kuhuisha turathi za wanachuoni wa zamani, sambamba na kuandaa kizazi cha wahakiki wenye uwezo wa kusoma hati za zamani, kuziripea na kuziandika upya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: