Kikosi cha Abbasi cha wapiganaji kinapongeza maafisa 9 waliohitimu kwenye chuo cha jeshi: tunatarajia watumikie kikosi na taifa lao

Kikosi cha Abbasi (a.s) kinapongeza maafisa 9 waliohitimu mafunzo ya ukakamavu ya themanini na tano yaliyo pewa jina la (mafunzo ya walinzi wa Iraq) katika chuo cha kijeshi.

Kiongozi wa kikosi Sayyid Maitham Zubaidi amesema “Maafisa wa kwanza kutoka Hashdu-Shaabi kuhitimu mafunzo hayo wapo tisa, tunatarajia huduma bora kutoka kwao katika kikosi na taifa lao.

Akaongeza kuwa “Lengo ni kuonyesha njia ya kuwa na kikosi cha Hashdu-Shaabi chenye maafisa mahiri waliohitimu kwenye chuo cha jeshi” akabainisha kuwa “Nimatumaini yetu kuona vikosi vingine vya Hashdu-Shaabi vinashiriki kwenye mafunzo haya katika awamu zijazo”.

Afisa wa chuo cha jeshi Blugedia Jenerali Faisal Aamiri amesema “Maafisa wa jeshi 578 wamehitimu kwenye chuo hiki”.

Akaongeza kuwa “Maafisa 9 miongoni mwao wanatoka kwenye kikosi cha Hashdu-Shaabi katika wapiganaji wa kikosi cha Abbasi, watashirikiana na wanajeshi wa serikali katika ulinzi wa taifa lao kwa ujuzi na damu zao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: