Kitengo cha usimamizi wa haram kimesema: Tunamisahafu inayokaribia elfu 10 ndani ya hara ya Abbasi

Kitengo cha usimamizi wa haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya kimesema kuwa kinamiliki karibu misahafu elfu kumi ndani ya haram tukufu ya Abbasi na kwenye sardabu zake.

Makamo rais wa kitengo hicho Shekhe Zainul-Aabidina Quraishi amesema “Ukumbi wa haram ya Abbasi, sardabu ya ndani na nje, una misahafu inayokaribia elfu kumi, vitabu vya ziara elfu tano na vitabu vya dua elfu ishirini, miongoni mwa vitabu hivyo ni Mafaatihu-Jinaani na Swahifatu-Sajadiyyah”

Katika stoo ya Atabatu Abbasiyya kuna vitabu vingi zaidi kushinda vilivyopo ndani ya haram tukufu, akabainisha kuwa “Sehemu ya vitabu hivyo hugawanywa kwenye misikiti na Husseiniyya baada ya kupewa ruhusa na uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: