Kitengo cha usimamizi wa haram ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeeleza utendaji wa idara ya misahafu ndani ya Ataba tukufu.
Makamo rais wa kitengo hicho Shekhe Zainul-Aabidina Quraishi amesema “Miongoni mwa majukumu ya idara ya misahafu ndani ya haram tukufu ni kutunza vitabu vya dua, ziara na misahafu sambamba na kufanyia ukarabati vitabu pale vinapo chakaa au kubadilisha na kuweka vitabu vipya”.
Kazi hizo hufanywa na watu waliobobea katika fani hiyo, majukumu ya idara yamepangwa kwa mwaka na nusu mwaka, mwaka jana tumekarabati vitabu kumi na tano.