Majmaa inaendelea na semina maalum za kanuni za usoamji

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea na semina maalum za kufundisha kanuni za usomaji wa Qur’ani.

Semina hizo zinasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.

Msimamizi wa semina hizo Shekhe Wasaam Sabti amesema “Hakika semina hizi ni sehemu ya mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini awamu ya saba, masomo ya Qur’ani wanayofundishwa yapo katika selibasi yao ya hauza”.

Akaongeza kuwa “Tunatarajia kupanua mradi huu zaidi, uwe na hatua nyingi”.

Akabainisha kuwa “Semina imefanywa katika taasisi ya Imamu Hassan Askariy (a.s) ikiwa na anuani isemayo (Semina ya Allamah Majlisi) kwa ushiriki wa wanafunzi wa hauza katika mji wa Najafu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: