Kitengo cha uhusiano kimehitimisha ratiba maalum ya wageni kutoka Ujerumani

Kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya, kimehitimisha ratiba maalum ya wageni wa kutuo cha Zaharaa (a.s) kutoka Ujerumani.

Mhadhiri Shekhe Haarith Daahi amesema “Vikao na mihadhara mbalimbali imetolewa kwa wageni waliokuja kutoka Ujerumani, mihadhara ilijikita katika kueleza mafundisho ya Mtume Muhammad na watu wa nyumbani kwake (a.s) Pamoja na mazingira ya mtu anayeishi katika jamii za watu wa magharibi”.

Akafafanua kuwa “Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya juhudi ya kudumisha mawasiliano na watu wa magharibi na kuwarahisishia upatikanaji wa elimu, ukizingatia mazingira ya jamii yao yanatofautiana na mazingira ya jamii yetu”.

Mmoja wa wageni hao kutoka Ujerumani amesema “Atabatu Abbasiyya imetupa mualiko wa kuja ziara nchini Iraq, tumefurahi sana kumtembelea Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), tumesikiliza mihadhara mingi yenye mada tofauti na muhimu kuhusu uhusiano wetu nchini Ujerumani, aidha tumetembelea miradi mingi ya Ataba tukufu ukiwemo mradi wa utengenezaji wa madirisha”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: