Kumbukumbu ya kifo cha Ummul-Banina (a.s).. Atabatu Abbasiyya inafanya majlisi ya kuomboleza kwa watumishi wake

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha mama wa Abulfadhil Abbasi (a.s) mama mtukufu mnusuruji wa familia Ummul-Banina (a.s).

Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala katika haram tukufu, imefunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na msomaji kutoka Majmaa-Ilmi bwana Ibrahim Abdallah na mawaidha yakatolewa na Shekhe Aqiil Mansuri.

Shekhe ameongea mambo mengi kuhusu Maisha ya mama huyu mtukufu, ambae Mwenyezi Mungu amemfanya kuwa mlango wa rehema na kukidhi haja za watu, aidha namna alivyo wapa kipaombele watoto wa Mtume kushinda watoto wake hadi akawatoa watoto wake waende kumlinda Imamu wao Abu Abdillahi Hussein (a.s), ambapo wote waliuawa kwa ajili hiyo, sambamba na mambo mengine mengi matukufu katika maisha yake (a.s), mwisho wa majlisi hiyo zikasomwa tenzi na kaswida za kuomboleza.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza msiba huu yenye vipengele vingi vya uombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: