Maukibu ya Kufa inatoa pole kwa Abulfadhil Abbasi kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Ummul-Banina (a.s)

Maukibu ya watu wa Kufa imetoa pole kwa Abulfadhil Abbasi (a.s)kufuatia kumbukumbu ya kifo cha mama yake Ummul-Banina (a.s) mbele ya kaburi lake takatifu katika mji wa Karbala.

Kiomgozi wa maukibu hiyo Sayyid Munafu Alkhafaji amesema “Vikundi vya Husseiniyya na mawakibu za mji wa Kufa zimeelekea Karbala kumpa pole Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na kumbukumbu ya kifo cha Ummul-Banina (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu, kimerahisisha uingiaji kwenye haram tukufu”, akatoa shukrani za dhati kwa Ataba tukufu kutokana na kazi kubwa inayofanya katika matukio ya kidini.

Washiriki wa maukibu wametoa pole kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia kifo cha mama yake mtukufu, wameeleza historia yake na namna alivyo jitolea yeye na watoto wake katika kumnusuru Imamu Hussein na Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: