Idara ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake inahuisha kumbukumbu ya kifo cha Ummul-Banina (a.s)

Idara ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imehuisha kumbukumbu ya kifo cha Ummul-Banina (a.s).

Majlisi hiyo imefanywa ndani ya Sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s), kwa kushirikiana na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya Ataba tukufu.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha kiongozi wa idara ya mahusiano na matukio ya kidini Sayyidah Rajaa Ali akatoa mhadhara uliojikita katika kueleza utukufu wa Ummul-Banina (a.s) na nafasi yake mbele ya Ahlulbait (a.s).

Idara ya wahadhiri ikaonyesha igizo lililopewa jina la (mwanamke katika mapambano), likaoyensha nafasi ya Ummul-Banina (a.s) wakati mateka waliporudi Madina.

Majlisi ikahitimishwa kwa kaswida na tenzi zilizoeleza utukufu wa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: