Miongoni mwa program ya kuwajengea uwezo watumishi wapya.. kitengo cha Dini kinatoa mafunzo ya Fiqhi

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinatoa mafunzo ya Fiqhi kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya kupitia program ya kujengea uwezo watumishi wapya.

Shekhe Abdulsataar Alhijami kutoka kitengo cha Dini amesema “Semina imekua na mada tofauti, yakiwemo masomo ya Fiqhi kutoka kitabu cha Alwajiiz kilicha andikwa na Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani, masomo ya Akhlaqi na Haqaaiq”.

Akaongeza kuwa “Semina imedumu kwa muda wa siku tano, lengo la semina hiyo ni kujenga uwezo wa masomo ya Dini kwa watumishi wapya na kuwafanya waweze kutekeleza wajibu wao kwa kufuata hukumu za kisheria”.

Kumbuka kuwa kila jambo analofanya mwanaadamu linahukumu ya kisheria, hivyo masomo haya yanasaidia kuwajengea uwelewa watumishi wetu wasije wakafanya mambo kinyume na sheria na kuingia katika makosa ya kuvunja sheria.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: