Kwa wanafunzi wa vyuo.. Majmaa-Ilmi inaendelea na vikao vya usomaji wa Qur’ani

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inaendelea kufanya vikao vya usomaji wa Qur’ani kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Kufa.

Vikao hivyo vinasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.

Kikao kimefunguliwa kwa usomaji wa Qur’ani tahfiidh na maswali yanayohusu kupima uhifadhi wa sura na aya za Qur’ani.

Kikao kimepambwa na mhadhara kutoka kwa Shekhe Shihabu Dini Al-Aamiri, uliofuatiwa na maoni na maswali kutoka kwa wanafunzi, na kuhitimishwa kwa kupiga kura na kugawa zawadi za kutabaruku kutoka kwenye malalo takatifu ya Abbasi.

Semina hii ni sehemu ya mradi wa Maahadi ya Qur’ani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi awamu ya tatu ya mwaka wa masomo (2022 – 2023) ambao hufanywa katika vyuo vikuu vya Najafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: