Ugeni kutoka wizara ya maji unajadiliana na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Ugeni kutoka wizara ya maji na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya wamejadili namna ya kushirikiana katika sekta ya utoaji wa mafunzo.

Ugeni umefanya kikao na kiongozi wa kamati kuu ya Ataba Dokta Abbasi Rashidi Mussawi na rais wa kitengo cha uboreshaji Dokta Muhammad Hassan Jaabir, wakajadili namna ya kushirikiana na kubadilishana uzowefu.

Miongoni mwa wageni hao ni Sayyid Twaha Dar’i Saadi, rais wa kitengo cha uboreshaji na Sayyid Osama Juma, wamejadili miradi ya Ataba, ikiwa ni pamoja na mradi wa shirika la Aljuud, Saaqi na shamba la kunazi.

Ugeni umepongeza uzowefu wa Atabatu Abbasiyya katika miradi ya umwagiliaji, na njia wanayotumia katika umwagiliaji, ukaonyesha kufurahishwa na maendeleo makubwa yaliyopo katika sekta ya ujenzi, wakasema kuwa watachukua uzowefu huo na Kwenda kuufanyia kazi wizarani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: