Hospitali ya Alkafeel.. imefanikiwa kuunganisha mfupa

Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel iliyopo Karbala, limefanikiwa kuunganisha mfupa wa mkuu (ugoko) wa kijana aliyepata ajali.

Daktari bingwa wa mifuta, Dokta Mustwafa Walidi amesema “Tumepokea mgonjwa aliyekua amevunjika mfupa wa mguu mara kadhaa kutokana na ajali ya gari, baada ya kumfanyia vipimo tukabaini kuwa anahitaji huduma ya kuunganisha mifupa”.

Akaongeza kuwa “Kijana alikua na hali mbaya, lakini baada ya kufanyiwa matibabu anaendelea vizuri kwa sasa” kumbuka mafanikio haya yanatokana na vifaa-tiba vya kisasa vilivyopo na umahiri wa madaktari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: