Chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya kongamano la kukumbuka shambulio la pili katika malalo ya Askariyaini

Chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya kongamano la kukumbuka shambulio la pili kwenye malalo ya maimamu wawili Askariyaini (a.s).

Kongamano hilo limefanywa kwa kushirikiana na kituo cha turathi za Samaraa chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Askariyya, limefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, halafu ukafuata ujumbe wa kiongozi wa kituo Dokta Mushtaqu Asadi, mbele ya rais wa chuo Dokta Nurisi Muhammad Shahidi Dahani, viongozi wa vitivo, walimu na mazuwaru.

Asadi ameongea kuhusu tukio la kulipuliwa kwa kubba la malalo ya maimamu wawili Askariyaini (a.s), na kazi kubwa iliyofanywa na wanachuoni watukufu ya kuzuwia mauwaji na uhamishwaji wa watu, akakumbusha hekima iliyochukuliwa na viongozi wa Dini na Maraajii pamoja na wananchi wa taifa hili ya kupambana na fitna.

Akaeleza uanzishwaji wa “kituo cha turathi za Samaraa” ambapo lengo kubwa ni kutoa elimu ya turathi na historia ya maimamu walioishi Samaraa, sambamba na kuonyesha historia ya mji huu wa kale katika uislamu.

Pembeni ya kongamano hilo lililofanywa katika ukumbi wa kitivo cha tiba ya meno, yamefanywa maonyesho ya Atabatu Askariyya yaliyokua na vitu mbalimbali yakiwemo baadhi ya mabaki ya shambulio la kubba na vielelezo vya picha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: