Majmaa-Ilmi imetangaza shindano la utafiti bora wa wahitimu wa masomo ya Qur’ani

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imetangaza shindano la kuchagua utafiti bora wa wahitimu wa masomo ya Qur’ani kupitia mradi wa Qur’ani katika vyuo vikuu na Maahadi.

Shindano hilo linasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.

Shindano linahusu wanafunzi wa vyuo vikuu vya Najafu na wale wanaosoma kwenye vitengo vya maarifa ya Qur’ani.

Mwisho wa kupokea mada ni tarehe (1/02/2023) na mwisho wa kuwasilisha tafiti ni (10/04/2023).

Shiriki kwenye shindano hili kupitia link ifuatayo:

https://forms.gle/7YDokqA4h8pwn2CE6
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: