Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na watu wa wilaya ya Tuzkharmatu katika mkoa wa Swalahu Dini imefanya mahafali za (mimbari za nuru) za Qur’ani.
Program hiyo imeandaliwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa, katika husseiniyya ya Rasuulul-Aadham (s.a.w.w) na kuhudhuriwa na wakazi wengi pamoja na viongozi wa hauza na wawakilishi wa Wakfu-Shia hapa mkoani.
Mahafali ilikua na mazingira mazuri ya utajo wa kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlulbait (a.s), wahudhuriaji wamesikiliza visomo tofauti kutoka kwa wasomaji mbalimbali, miongoni mwa wasomaji hao ni Sayyid Hassanaini Halo ambaye ni msomaji wa Ataba mbili tukufu na Muhammad Ridha Zubaidi kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu.
Ameshiriki pia muimbaji kijana Muhammad Baaqir Qahtwani, mahafali hii imerushwa na chanel ya Qur’ani tukufu katika luninga za Karbala.