Majmaa-Ilmi inapongeza wanafunzi 60 walioshiriki kwenye semina za Qur’ani

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inapongeza wanafunzi 60 walioshiriki kwenye semina za Qur’ani, ambapo wamefundishwa usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu.

Semina hizo husimamiwa na idara ya usomaji katika Maahadi ya Qur’ani tukufu mjini Najafu chini ya Majmaa.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na mwanafunzi aliyefanya vizuri wakati wa semina Hussein Habubi, ikafuatiwa na ujumbe kutoka kwa mkuu wa Maahadi Sayyid Muhandi Almayali, ametoa pongezi nyingi kwa washiriki wa semina.

Dokta Karim Zubaidi amepongeza idara ya Maahadi kwa kazi kubwa inayofanya ya kufundisha Qur’ani na mwenendo wa Ahlulbait (a.s) katika jamii.

Mwisho wa mahafali hiyo washiriki wa semina wakapewa vyeti na zawadi za kutabaruku na Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: