Hospitali ya Alkafeel: Tumepata mafanikio makubwa katika upasuaji wa kutibu tatizo la sauti

Hospitali ya rufaa Alkafeel katika mkoa wa Karbala, imepata mafanikio makubwa katika upasuaji wa kutibu tatizo la sauti kwa wanaume na wanawake.

Daktari bingwa wa masikio, pua na koo katika hospitali hiyo, Dokta Aadil Masudi amesema: “Hakika upasuaji wa kutibu tatizo la sauti na kubadilisha kutoka sauti ya kiume kuwa sauti ya kike haukuwa ukifanyika hapa Iraq, sisi tumeanza kuufanya tangu miaka miwili iliyopita baada ya kupata vifaa-tiba vya kisasa na wataalamu mahiri, umefanyika kwa mafanikio makubwa”.

Akaongeza kuwa: “Upasuaji wa mwisho tulimfanyia kijana mwenye umri wa miaka (28) alikuana tatizo la sauti, na alikua amesha tumia dawa nyingi bila mafanikio”.

Tulifanya upasuaji kwa kutumia vifaa-tiba na mbinu za kisasa, akasisitiza kuwa “Upasuaji umefanikiwa na mgonjwa amerudi katika hali ya kawaida akiwa na afya nzuri, vifaa-tiba vya kisasa na umahiri wa madaktari ndio msingi wa mafanikio”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: