Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa, itakarabati soko la Alawi na maeneo yanayozunguka soko hilo.
Opresheni hiyo ni sehemu ya mradi wa upanuzi na ujenzi unaoshuhudiwa katika mji wa Karbala na maeneo yanayozunguka haram tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Soko la Alawi lipo karibu na Atabatu Abbasiyya tukufu ni soko muhimu katika mji wa Karbala, kwani ni soko la kihistoria kwa wakazi wa mji huu na mazuwaru, pia linaumuhimu mkubwa kiuchumi.