Wajibu wa kijana.. kitengo cha uboreshaji kinatoa mafunzo kuhusu uchukuaji wa maamuzi

Kitengo cha uboreshaji na maendeleo katika Atabatu Abbasiyya kinafanya warsha kuhusu wajibu wa kijana katika Ataba tukufu.

Mhadhiri wa warsha hiyo Sayyid Farasi Shimri amesema “Warsha hii ni sehemu ya program ya utatuzi wa changamoto, washiriki wanafundishwa namna ya kufanya maamuzi ya haraka katika kutatua changamoto, sambamba na kuangalia vipaombele na kufanya maamuzi sahihi, sawa maamuzi hayo yanahusu mtu binafsi au mfumo”.

Akaongeza kuwa “Wamefundishwa mada nyingi, ikiwa ni pamoja na kutambua maamuzi, namna ya kufanya maamuzi, mbinu za maamuzi, mafunzo hayo yanafanywa ndani ya ukumbi wa Nafidhul-Baswirah yatadumu kwa muda wa siku sita, wanakaa darasani saa tano kila siku”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: