Hospitali ya Alkafeel.. kijana katibiwa ugonjwa wa kupooza, na viungo vyake vinafanya kazi

Jopo la madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel limefanikiwa kurudisha utendaji wa viungo vya kijana vilivyokua vimepooza.

Daktari bingwa wa matatizo ya uti wa mgongo, Dokta Mhammad Zaarii amesema “Kijana alikua amepooza viungo kwa sababu ya kubana kwa mshipa wa fahamu unao unganisha kichwa na sehemu zingine za muili, hivyo alikua anahitaji upasuaji wa haraka ili kuzuwia asipooze muili mzima”.

Jopo la madaktari limemfanyia upasuaji wa kupanua njia ya mshipa na kuweka uteute kwenye baadhi ya mishipa ya kichwa, akasema kuwa hakupata shida yeyote wakati na baada ya upasuaji, ameruhusiwa kurudi nyumbani akiwa na afya nzuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: