Kitengo cha uboreshaji kinaendelea na ratiba ya kuwajengea uwezo watumishi wapya

Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya, kinaendelea na ratiba ya kuwajengea uwezo watumishi wapya.

Kiongozi wa habari na mahusiano Sayyid Anwaru Sarhani amesema “Ratiba hii inaendelea kwa wiki ya tatu katika mwezi wa tano, lengo ni kuwajengea uwezo watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kuwa “Ratiba inahusisha shughuli za kitamaduni, mihadhara ya kidini, mashindano mbalimbali, ziara za mapumziko na kidini kwa lengo la kuimarisha mahusiano baina ya watumishi”.

Kwa mujibu wa Sarhani “Ratiba hii inahusisha kutembelea zaidi ya miradi 150 ya Atabatu Abbasiyya, ikiwa ni pamoja na kiwanda cha kutengeneza madirisha, kiwanda cha Aljuud, kiwanda cha Alkafeel, shamba la kunazi na miradi mingine”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: