Kituo cha utamaduni wa familia kinafanya program ya kitamaduni katika shule ya Fadaki-Zaharaa (a.s)

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kinafanya program ya kitamaduni ya (Nuru juu ya nuru) katika shule ya Fadaki-Zaharaa (a.s) ya wasichana.

Bibi Adhraa Ahmadi amewasilisha mada isemayo (siri ya furaha) na bibi Sundusi Muhammad ametoa mada isemayo (unaona nini?) halafu ikafuata program ya (kutoka kwenu hadi kwenu) ya kujibu maswali ya washiriki.

Kituo kinafanya kazi kubwa ya kufundisha jamii mwenendo sahihi sambamba na kufuata utamaduni wa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: