Katika kuonyesha thamani ya msaada wake kwa vyombo vya ulinzi na usalama.. polisi wa Karbala wakabidhi zawadi kwa idara ya hospitali ya Alkafeel

Idara ya polisi ya mkoa wa Karbala imekabidi zawadi kwa idara ya hospitali ya rufaa Alkafeel, kutokana na msaada wake kwa vyombo vya ulinzi na usalama.

Zawadi hiyo imetolewa baada ya ziara ya kiongozi wa polisi na mkuu wa kitengo cha mashahidi na majeruhi kutembelea hospitali ya Alkafeel, wametoa shukrani nyingi kwa uongozi wa hospitali kutokana na namna hospitali inavyojali na kuhudumia askari wanaojeruhiwa kwenye uwanja wa mapambano.

Idara ya hospitali imefurahishwa na ziara hiyo na imeahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kutibu majeruhi, aidha imepongeza kazi kubwa inayo fanywa na vyombo vya ulinzi na usalama ya kudumisha amani na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: