Kuhitimisha shughuli za siku ya tatu ya kongamano la Ruhu-Nubuwah

Idara ya shule za dini za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya, zimemaliza shughuli za siku ya tatu ya kongamano la kimataifa Ruhu-Nubuwah awamu ya tano.

Kiongozi wa idara bibi Bushra Kinani amesema “Shughuli za siku ya tatu ya kongamano linalofanywa katika chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kauli mbiu isemayo (Bibi Zaharaa -a.s- ni athari tukufu ya kujivunia), zimefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyofuatiwa na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukasomwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya (Lahnul-Ibaa)”.

Akaongeza kuwa “Ratiba ya siku ya tatu imehusisha maonyesho ya filamu na shughuli zinazofanywa na taasisi za Atabatu Abbasiyya kisha yakafuata maonyesho ya vitabu”.

Akabainisha kuwa “Nadwa ya kwanza ilikuwa na anuani isemayo (Utandawazi wa kimagharibi na athari zake katika Dini), mada hiyo iliwasilishwa na Sayyid Hashim Murtadhwa Almilani, nadwa ya pili ikawa na mada isemayo (Mwanamke na swali la utambulisho, utafiti katika mfumo wa familia) iliyotolewa na Shekhe Hassan Ahmadi Alhadi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: