Kuhitimisha kongamano la kimataifa Ruhu-Nubuwah awamu ya tano

Idara ya shule za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya imehitimisha kongamano la Ruhu-Nubuwah awamu ya tano.

Hafla ya kuhitimisha kongamano hilo lililokuwa na kaulimbiu isemayo (Bibi Zaharaa -a.s- ni athari takatifu ya kujivunia) imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyo fuatiwa na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq.

Halafu ukafuata ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya uliowasilishwa na mjumbe wa kamati kuu Sayyid Abbasi Rashidi Mussawi.

Kiongozi wa idara ya wanawake bibi Bushra Kinani amehutumia hafla hiyo, amesema kuwa “Mwaka wa tano mfululizo tunafanya kongamano hili, tunapata nafasi ya kumjadili bibi Zaharaa (a.s) katika nyanja tofauti za Maisha yake”.

Akasisitiza kuwa “Yatupasa kushikamana na Qur’ani tukufu pamoja na mafundisho ya Ahlulbait (a.s)”.

Washiriki wa kongamano hilo pia walipata nafasi ya kutoa ujumbe, miongoni mwa waliozungumza ni mwalimu kutoka chuo kikuu cha Basra bibi Salma Abdulhamidi, amesema “Kongamano la Ruhu-Nubuwah ni la kipekee, hutolewa maelekezo mbalimbali yanayosaidia jamii ya wanawake na dunia kwa ujumla”.

Katika halfa hiyo washindi wa mashindano mbalimbali yaliyofanywa wakati wa kongamano wamepewa zawadi, ikumbukwe kuwa kulikua na shindano la mashairi ufundi wa kazi za mikono, picha, uchoraji na shindano la tafiti za kongamano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: