Idara ya maelekezo ya Dini imefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya bibi Zaharaa (a.s)

Idara ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya bibi Swidiqah Fatuma Zaharaa (a.s).

Kiongozi wa idara bibi Adhraa Shami amesema “Hafla ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu na dua, imepata mahudhurio makubwa na kulikua na mambo mbalimbali ya kidini na kitamaduni”.

Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya tukufu huyapa kipaombele matukio ya kuadhimisha kumbukumbu za mazazi na vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), jambo hilo lipo kwenye ratiba ya matukio ya mwaka”.

Akabainisha kuwa “Katika hafla hiyo imeelezwa historia ya bibi Zaharaa (a.s) iliyofuatiwa na mashairi na tenzi tofauti kutoka idara ya wahadhiri na shule ya Fadak sambamba na kugawa zawadi kwa washindi wa shindano la pambo takatifu”.

Hafla ikahitimishwa kwa kuwapa zawadi wastafu wa idara ya Zainabiyya katika Atabatu Abbasiyya, zawadi hiyo imekabidhiwa na kiongozi wa idara bibi Suzan Ahmadi, kama sehemu ya kuonyesha thamani ya mchango mkubwa waliotoa katika kumtumikia Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru wake wakati wote walipokua kazini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: