Maazimio ya kongamano la Ruhu-Nubuwah awamu ya tano

Kongamano la kimataifa Ruhu-Nubuwah awamu ya tano lililoandaliwa na idara ya shule za Alkafeel tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya limetoka na maazimio kadhaa.

Kongamano hilo lilikua na kauli mbiu isemayo (Bibi Zaharaa -a.s- ni athari takatifu ya kujivunia) na maazimio kadhaa yamependekezwa, miongoni mwa maazimio hayo ni kupanua wigo wa tafiti kwa kuangazia wanawake wa nyumba ya Mtume, hasa bibi Zahara, bibi Khadija na bibi Zainabu (a.s).

Kongamano limetoa wito wa kuongeza ushirikiano na shule za sekula na kuomba waandishi wa ndani na nje ya Iraq waifanyie utafiti hutuba ya Fadakiyya iliyotolewa na bibi Zaharaa (a.s), na kushawishi wizara ya malezi na elimu kuiweka kwenye mtaala wa shule za sekondari (upili).

Imesisitizwa kuandaa vielelezo kwa kushirikiana na kituo cha masomo ya kimkakati chini ya Atabatu Abbasiyya, kwa ajili ya kulinda familia zisiharibike, na kusaidia vyombo vya Habari vitangaze vipengele vya kongamano, halafu kiandaliwe kikosi-kazi kwa ajili ya ufuatiliaji ndani na nje ya Iraq na kupanua wigo wa ushiriki.

Washiriki wamehimiza umuhimu wa kushirikiana kwa taasisi za kitamaduni zilizo chini ya Ataba tukufu, na kupanga nyakati za makongamano ya kielimu, ili kusiwe na mgongano kwa watafiti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: