Majmaa-Ilmi imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani katika chuo kikuu cha Karbala

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani kwenye chuo kikuu cha Karbala, katika mfululizo wa ratiba ya (mimbari za nuru).

Hafla hiyo imesimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa, kwa kushirikiana na kitivo cha malezi na sayansi ya mwanaadamu hapo chuoni.

Imefanywa sambamba na maadhimisho ya kuzaliwa kwa bibi Zaharaa (a.s), Qur’ani imesomwa kwa vikundi na mtu mmoja mmoja pamoja na tenzi mbalimbali, miongoni mwa wasomaji ni Sayyid Hasanaini Halo na msomaji wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Ammaar Alhilly.

Usomaji wa vikundi umefanywa na wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji, aidha muimbaji wa husseiniyya Sayyid Muhammad Baaqir Qahtwani pia ameshiriki katika uimbaji wa tenzi.

Rais wa Majmaa-Ilmi Dokta Mushtaqu Ali amehudhuria hafla hiyo, na baadhi ya wadau wa Qur’ani, watumishi wa chuo na wanafunzi, mazingira yalikua tulivu yaliyojaa visomo vya Qur’ani na utajo wa Ahlulbait (a.s).

Halfa hii inalenga kusambaza elimu ya usomaji wa Qur’ani katika vyuo vikuu na kuibua vipaji vya usomaji wa Qur’ani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: