Katika mji wa Dhiqaar.. Atabatu Abbasiyya inaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Zaharaa (a.s)

Atabatu Abbasiyya tukufu imeadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa bibi Zaharaa (a.s) katika mkoa wa Dhiqaar.

Kiongozi wa idara ya wahadhiri katika Ataba tukufu Shekhe Abduswahibu Twaiy amesema “Hafla ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na surat Faatiha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha zikasomwa tenzi na Mula Ammaar Alkinani kuhusu kumbukizi ya kuzaliwa kwa nuru ya ardhi na mbora wa wanawake wa duniani bibi Fatuma Zaharaa (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Huwa tunafanya maadhimisho kama haya katika kumbukizi zote za watu wa nyumba ya Mtume (a.s) kwenye mikoa tofauti ya Iraq”, akabainisha kuwa “Tumefanya hafla katika wilaya ya Diwaya ndani ya Husseiniyya ya Fatuma Zaharaa (a.s) iliyokua na mahudhurio makubwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: