Chuo kikuu cha Al-Ameed kimesema: Maabara yetu inalingana na maabara za vyuo vikuu vya kimataifa

Makamo kiongozi wa kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Ali Dhulfiqaar Albaswam amesema kuwa, maabara ya chuo inamitambo ya kisasa sawa na maabara zilizopo kwenye vyuo vikuu vya kimataifa.

Akaongeza kuwa “Kitivo cha udaktari kinaubora mkubwa sawa na vyuo vya kimataifa”.

Katika idara ya upimaji kuna mitambo ya kisasa inayomuwezesha mwanafunzi kutambua muili wa mwanaadamu kwa ndani na nje, sambamba na kumfundisha njia za utoaji wa huduma ya kwanza na namna ya upasuaji.

Makamo kiongozi wa chuo akasema “Maabara inamitambo ya kisasa zaidi na vitanda vyenye ubora wa kiwango cha juu kabisa”.

Kwa mujibu wa Albaswam hakika chuo kinaenda sambamba na maendeleo ya kisasa kwa kutumia vifaa vya kisasa zaidi kwa mwanafunzi na mwalimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: