Majmaa-Ilmi inaendelea na ratiba ya kitablighi katika mkoa wa Swalahu Dini na Kirkuki

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea na ratiba ya Tablighi iitwayo (Yubalighuna) katika mkoa wa Kirkuki na Swalahu Dini.

Ratiba hiyo inasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Najafu chini ya Majmaa.

Ratiba inalenga taasisi kumi na nne za Qur’ani katika wilaya tano, ambazo ni makao makuu ya mkoa wa Kirkuki, Daquuq, Tuzkharmatu, Tazah na Aamirli, makumi ya wasomaji wa Qur’ani wanashiriki katika ratiba hii.

Program inahusisha utoaji wa mihadhara kwa wanafunzi wa hauza pamoja na jinsi ya kuishi na Qur’ani katika siku yako na vikao vya majadiliano, sambamba na kufanya nadwa za kujadili hali halisi ya Qur’ani katika mikoa miwili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: