Shule za Alkafeel za wasichana zinafanya semina ya Qur’ani

Idara ya shule za Alkafeel za Dini upande wa wasichana katika Atabatu Abbasiyya inafanya nadwa yenye anuani isemayo (Namna ya kutafakari katika Qur’ani tukufu).

Shule kadhaa zilizochini ya Atabatu Abbasiyya zimeshiriki kwenye nadwa hiyo, muendeshaji mkuu wa nadwa hiyo ni Dokta Radhiya Sajaadi kutoka Iran na Dokta Radhiya Hussein Alkhayaatu kiongozi wa shule ya Fadak.

Kuhusu lengo la nadwa amesema “Inalenga kufahamu Qur’ani na miujiza iliyosaidia kufikiwa lengo la Mwenyezi Mungu la kushushwa kwa Qur’ani tukufu”.

Mada za nadwa zimejikita katika kutambulisha Qur’ani, kufanya tafakari na zimefafanuliwa kwa undani aya mbili tukufu, aya ya kwanza ipo katika surat Muhammad aya ya 24 na nyingine katika surat Swaad aya ya 29.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: