Majmaa-Ilmi inaendesha semina mbili za Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inaendesha semina mbili za Qur’ani, kupitia mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini awamu ya sita.

Semina hizo zinasimamiwa na idara ya hauza katika Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.

Msimamizi wa semina hizo Shekhe Wasaam Sibti amesema “Moja ya semina hizo imefanywa katika madrasa ya Sayyid Hakiim, na ikapewa jina la semina ya Shekhe Abu Hassan Isfahaani, na nyingine imefanywa katika Majmaa-Alawiy kwa jina la Shekhe Muhammad Jawadi Albalaghi iliyokua na washiriki (40)”.

Akasema: “Tumesha fanya zaidi ya semina kumi na tatu kupitia mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini, zaidi ya wanafunzi (250) wamenufaika na semina hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: