Majmaa-Ilmi imehitimisha ratiba ya kitablighi katika mkoa wa Kirkuki na Swalahu Dini

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imehitimisha ratiba ya kielimu isemayo (Yubalighuna) katika mkoa wa Kirkuki na Swalahu Dini.

Ratiba hiyo imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.

Mkuu wa Maahadi Sayyid Muhandi Almayali anasema “Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na mawasiliano ya kielimu na kimaarifa, baina ya taasisi za Qur’ani zilizopo mikoani”.

Akaongeza kuwa “Ratiba ya (yubalighuna) inaendelea kudumisha mawasiliano na Maahazi za mikoani”.

Almayali akabainisha kuwa “Katika siku ya tatu na ya mwisho, imefanywa hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Fatuma Zaharaa (a.s) iliyohudhuriwa na taasisi (13) za Qur’ani mkoani Kirkuki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: